1 Aprili 2015 - 18:27
Obama ampongeza Buhari

Rais mteule wa Nigeria Muhammadu Buhari ameapa leo kwa atachukua hatua kali dhidi ya kundi la Boko Haram na kuahidi kufanya maridhiano na kuunda serikali itakayojumuisha watu wa maeneo yote nchini humo katika hotuba yake ya kwanza tangu kushinda uchaguzi.

Buhari  amesema  huu  ni  wakati  wa  kuponya  machungu ,  na kuongeza  kwamba  Wanigeria  wameweka  kando  taifa  la  chama kimoja  na  kukumbatia  demokrasia.

Wakati  huo  huo  rais  wa  Barack Obama  wa  Marekani  amemsifu rais Goodluck Jonathan  leo kwa  kukubali  kushindwa  katika uchaguzi  wa  rais  ambao  amesema  umeonesha  nia  ya  Nigeria kutekeleza  misingi  ya  demokrasia.

Obama  amesema  katika  taarifa  kwamba  rais  Jonathan ameweka  maslahi  ya  taifa  lake  kwanza  kwa  kukubali  kushindwa katika  uchaguzi  na  kumpongeza  rais  mteule Muhammadu Buhari kwa  ushindi.

Nae katibu  mkuu  wa  Umoja  wa  mataifa  Ban Ki-moon nae amempongeza  rais  mpya  wa  Nigeria  Muhammadu Buhari kwa ushindi  wake  na  kusema  kwamba  uchaguzi  huo  ni  ushahidi  wa ukomavu katika  demokrasia  nchini  Nigeria.